Taarifa kwa Vyombo vya Habari
PSI/Tanzania yasambaza kondomu milioni 72
Dar es Salaam September 7, 2011 …Shirika lisilokuwa la kiserikali linalotoa elimu na huduma za afya nchini – PSI/Tanzania limesambaza kondomu za kiume milioni 72 nchini kote katika kipindi cha mwaka jana. Katika kipindi cha mwaka 2009, Kondomu zilizosambazwa ni 68,600,000.
Kondom hizo zilisambazwa kupitia kwa wanunuzi wa jumla wa mikoa (Regional Distributors) ambao wanawajibika kusambaza bidhaa hizo kupitia kwa wateja wajumla.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja kwa wahariri na waandishi waandamizi wa vyombo vya habari nchini, Mkurugenzi Mtendaji wa PSI/Tanzania Romanus Mtung’e alisema kiasi hicho kilichosambazwa kimechakia kwa kiasi kikubwa katika kupumbukuza maambukizi mapya ya UKIMWi nchini.
“Kwa PSI ongezeko la matumizi ya kondomu hapa nchini yanatupatia mwelekeo mzuri kuwa hivi sasa wananchi walio wengi wanaouelewa kuhusiana na ugonjwa wa Ukimwi, jinsi gani ya kujilinda ikiwa ni pamoja na matumizi ya mipira ya kiume na ya kike,” alisema Mtung’e.
Aliongeza kusema kuwa kupanda kwa uelewa wa Watanzania kuhusiana na ugonjwa wa UKIMWI kunatokana na ushirikiano mkubwa uliopo kati ya vyombo vya habari na serikali pamoja na mashirika yote yaliyopo katika mapambano dhidi ya UKIMWI.
“Leo tupo hapa ili kubadilishana mawazo na kupeana taarifa muhimu juu ya kile ambacho sisi tunakifanya, hii siyo mara ya kwanza kwa sisi kukutana na wahariri au waandishi wa habari, tumekuwa tukifanya hivyo kwa sababu tunatambua umuhimu na ushiriki wenu mzuri katika mapambano dhidi ya UKIMWI.”
Alisema mafanikio ambayo yameanza kupatikana hapa nchini ya kushuka kwa kiwango cha maambukizi ya UKIMWI kutoka asilimia 7.8 mwaka 2008 hadi kufikia asilimia 5.7 mwaka jana yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na elimu inayotolewa na wadau mbalimbali kupitia vyombo vya habari.
“Watu wa habari na vyombo vya habari ni wadau muhimu sana katika mapambano dhidi ya UKIMWI kwasababu wanawasiliana na jamii moja kwa moja na kwa wakati mmoja na PSI/Tanzania wanalitambua jambo hilo na wakati wote tupo tayari kushirikiana nanyi katika kufikisha elimu sahihi kuhusu UKIMWI kwa wanajamii.
“Taarifa za kushuka kidogo kwa kiwango cha maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kunaenda sambamba na ongezeko la matumizi ya kondomu hapa nchini, hivyo PSI imejizatiti katika kuendeleza na kubuni mbinu zaidi ambazo zitaongeza zaidi matumizi sahihi naya kila mara ya kondomu, kama ambavyo watendaji wetu wa Program ya UKIMWI watakavyotueleza hapa.”
Taarifa zaidi wasiliana:
John Wanyancha
Mkurungenzi wa Ushirikiano PSI/Tanzania
Simu: 0784 723236
Barua pepe: jwanyancha@psi.or.tz